LIVE STREAM ADS

Header Ads

Dhahabu “FEKI” yakamatwa Mwanza na Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Vyombo vya ulinzi na usalama vimewanasa watuhumiwa kadhaa katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga wakiwa kwenye harakati za kusafirisha dhahabu "FEKI" kwenda nje ya nchi.

Akizungumza na wafanyabiashara wa madini jijini Mwanza Agosti 08, 2019, Waziri wa Madini Doto Biteko alisema kiasi cha kilo 6.255 za dhahabu hiyo “FEKI” zilikamatwa Mkoa Mwanza huku kilo 4.58 zikikamatwa mkoani Shinyanga.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akizungumzia kukamatwa kwa dhahabu "feki" katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila
 Watendaji wa Wizara ya Madini wakionesha vipande vya dhahabu "feki" iliyokamatwa.
 Sehemu ya vipande vya dhahabu "feki" vilivyokamatwa katika mikoa ya Mwanza na Geita ikiwa kwenye harakati za kusafirihwa kwenda nje ya nje kuwauzia wafanyabiashara jambo ambalo ni utapeli na kinyume cha sheria za nchi.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.