LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya TAHA yaibuka kidedea Maonesho ya Nane Nane 2019

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Taasisi ya kilimo cha mboga mboga na matunda TAHA (Tanzania Horticultural Association) imeibuka nafasi ya kwanza miongoni mwa taasisi za utafiti wa mbegu bora za kilimo katika Maonesho ya Nane Nane 2019 yaliyofanyika kwa Kanda ya Ziwa Magharibi katika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza.

Baada ya kupokea kikombe kutoka kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella kwenye kilele cha maadhimisho hayo Agosti 08, 2019, Meneja Mkuu Uendeshaji TAHA Simon Mlay alisema zaidi ya wananchi/ wakulima elfu moja wamepata elimu kupitia shamba darasa la taasisi hiyo hatua ambayo imechochea ushindi huo.

Naye Mtaalamu wa TEHAMA na Utunzaji Kumbukumbu kutoka TAHA, Dismas Massawe alisema taasisi hiyo imejikita kutoa elimu na mbinu bora za kilimo kwa wakulima wadogo ili wakue kutoka kilimo cha mazoea kwenda kwenye kilimo chenye tija.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Meneja Mkuu Uendeshaji kutoka taasisi ya TAHA, Simon Mlay akipokea kikombe cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Meneja Mkuu Uendeshaji kutoka taasisi ya TAHA, Simon Mlay akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Christopher Kadio baada ya kupokea kikombe cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
 Meneja Mkuu Uendeshaji kutoka taasisi ya TAHA, Simon Mlay akizungumza na wanahabari kuhusu Maonesho ya Nane Nane 2019.
 Mtaalamu wa TEHAMA na Utunzaji Kumbukumbu kutoka TAHA, Dismas Massawe akieleza namna taasisi hiyo inavyowaelimisha wakulima wa mboga mboga na matunda.
Tazama BMG Online TV haoa chini

No comments:

Powered by Blogger.