Header Ads

MWAUWASA wazungumzia mabadiliko ya bei mpya za maji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) imetoa ufafanuzi kuhusu mabadiliko mapya ya ankra za maji huku ikitumia fursa hiyo kuwaelekeza wafanyabiashara wa maji kwamba bei elekezi kwa ndoo moja ya maji yenye ujazo wa lita 20 ni shilingi 50 tu.

Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga alitoa ufafanuzi huo Agosti 09, 2019 kwenye ziara ya waandishi wa habari mkoani Mwanza kutembelea miradi mbalimbali ya maji inayosimamiwa na mamlaka hiyo ili kujifunza utendaji kazi wake.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga akitoa ufafanuzi kwa wanahabari (hawako pichani)  kuhusu miradi ya maji inayosimamiwa na mamlaka hiyo pamoja na ongezeko la bei mpya ya maji.
 Wanahabari walitembelea eneo hili la mradi wa maji Capripoint jijini Mwanza kujifunza maji yanavyosafishwa na kutibiwa kabla ya kumfikia mtumiaji.
 Mradi wa maji MWAUWASA Capripoint jijini Mwanza.
Wanahabari pia walitembelea mradi mpya wa maji Nyahiti wilayani Misungwi na kushuhudia kwa mara ya kwanza mashine za kusukuma maji zikiwashwa kwenye mradi huo.
 Tenki kubwa la kusambazia maji katika mji wa Misingwi kutoka chanzo cha maji Nyahiti.
 Ziara hii iliratibiwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) ikilenga pia kuimarisha mahusiano na MWAUWASA.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.