LIVE STREAM ADS

Header Ads

“Nane Nane kitaifa ikifanyika Mwanza mtajua mchezo ukoje” RC Mongella

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ametoa ridhaa ya maonesho ya bidhaa za kilimo, ufugaji na uvuvi (Nane Nane) 2019 katika Kanda ya Ziwa Magharibi kuendelea hadi jumapili Agosti 11, 2019.

Mongella ameyasema hayo Agosti 08, 2019 alipokuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha kitaifa cha maonesho hayo yanayofanyika kwa Kanda ya Ziwa Magharibi katika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza, yakihusisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel baada ya kuwasili kwenye maonesho ya Nane Nane Nyamhongolo jijini Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akisalimiana na baadhi ya washiriki wa maonesho hayo wakati akikagua manda yao.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiteta na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majitaka na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUASA) alipotembelea banda la mamlaka hiyo kubwa zaidi akieleza kushtushwa na ongezeko la ankra mpya za maji.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikagua banda la kiwanda cha kutengeneza bidhaa za nguo ikiwemo vitenge MWATEX.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.