LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi wilayani Tarime waomba Shule waliyoijenga ifunguliwe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Wakazi wa Kijiji cha Muriba kilichopo Wilaya Tarime mkoani Mara wameiomba Serikali kuwasaidia kufungua Shule ya Sekondari Muriba waliyoijengwa kwa nguvu zao ili ianze kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wanatembea umbali mrefu kusaka elimu.

Walitoa ombi hilo Agosti 05, 2019 kwenye mdahalo wa utoaji elimu ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hususani wa kike uliofanyika katika Kata ya Muriba wilayani humo.

Mdahalo huo ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo mpango mkakati wa kitaifa wa kupambana na aina zote za ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA) ambapo Wilaya Tarime inatekeleza mpango huo kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana (KIVULINI).
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Muriba wilayani Tarime akizungumza kwenye mdahalo wa kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia ambapo alitoa ombi la kufunguliwa Shule ya Sekondari Muriba ili kuondoa adha ya watoto wao kutembea umbali mrefu kusaka elimu.
 Mwonekano wa choo chenye matundu manne katika Shule ya Sekondari Muriba ambayo bado haijaanza kupokea wanafunzi.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya Wilaya Tarime, Sunday Magacha akitolea ufafanuzi suala la kufunguliwa Shule ya Sekondari Muriba.
 Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akisisitiza jambo kwenye mdahalo huo.
 Jumbe mbalimbali kupitia mabango ya wanaharakati wa kujitolea ngazi ya jamii waliojengewa uwezo na Shirika la KIVULINI ili kutoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia wilayani Tarime.
wanaharakati wa kujitolea ngazi ya jamii waliojengewa uwezo na Shirika la KIVULINI wakiingia kwenye mdahalo huo huku wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali za kuzuia ukatili wa kijinsia.
 Waendesha bodaboda wa Muriba pia waliungana na pamoja kuhakikisha kampeni ya kutokomeza ukatili wilayani Tarime inafikia matokeo chanya katika jamii.
 Taswira mdahalo/ kampeni ya kutoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia Kata ya Muriba wilayani Tarime.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.