LIVE STREAM ADS

Header Ads

Viongozi watakiwa kuchukua hatua kunusuru wanafunzi wilayani Tarime

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Viongozi hususani wa Serikali kuanzia ngazi ya Kijiji wametakiwa kuchukua hatua ili kupambana na utoro kwa wanafunzi katika Shule mbalimbali za Msingi na Sekondari zilizopo Wilaya Tarime mkoani Mara unaochangia kudhorotesha kiwango cha elimu.

Rai hiyo ilitolewa jana Agosti 05, 2019 kwenye mdahalo wa utoaji elimu ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hususani wa kike uliofanyika katika Kata ya Muriba wilayani humo.

Mdahalo huo ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo mpango mkakati wa kitaifa wa kupambana na aina zote za ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA) ambapo Wilaya Tarime inatekeleza mpango huo kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana (KIVULINI).
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Taswira ilivyokuwa kwenye kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Kata ya Muriba wilayani Tarime.
 Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akitoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo kuachana na mila ya ukeketaji kwenye mdahalo huo.
 Afisa Elimu Kata ya Muriba wilayani Tarime, Mwl. Kefa Odao akitoa rai kwa wazazi na walezi katika Kata hiyo kuacha kuwapangia majukumu watoto wao siku za masomo hatua inayochochea ongezeko la utoro mashuleni.
 Viongozi na watendaji mbalimbali wilayani Tarime wakifuatilia mdahalo huo.
 Waendesha bodaboda katika Kata ya Muriba wilayani Tarime waliunga mkono juhudi ya kupambana na ukatili wa kijinsia hususani kupambana na mimba na ndoa kwa wanafunzi.
 Wanaharakati wa kujitolea waliopewa mafunzo na shirika la KIVULINI kusaidia utoaji elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia ngazi ya jamii wakiongoza maandamano ya kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu kupinga aina zote za ukatili katika jamii.
 Wanaharakati wa kujitolea wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kupinga aina zote za vitendo vya ukatili katika jamii.
 Wanafunzi wakitoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia kwa njia ya nyimbo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.