LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Mkuu ashiriki mazishi ya Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiaga mwili wa marehemu Natalia Bahati Kilangi ambaye alikuwa mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, leo Jumatano Agosti 07, 2019 katika Mtaa wa Luchelele jijini Mwanza.

Marehemu Natalia Bahati Kilangi aliyezaliwa Februari 15, 1979 alifariki dunia jumamosi Agosti 03, 2019 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando baada ya kupatwa na shinikizo la damu/ kiharusi. 

Kabla ya kupatwa na mauti, marehemu Natalia Bahati Kilangi alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SAUT ambapo ibada ya mazishi imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki na Geita, Askofu Flavian Kassala ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC).
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella wakiuaga mwili wa marehemu Natalia Bahati Kilangi ambaye alikuwa Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi.
 Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Madini, Doto Biteko pamoja na Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella wakiuaga mwili wa marehemu, Natalia Bahati Kilangi ambaye alikuwa mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi.
 Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Mwanza, Renatus Nkwande akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Natalia Bahati Kilangi ambaye alikuwa mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Natalia Bahati Kilangi ambaye alikuwa mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi.
 Wakuu wa Mikoa waliohudhuria mazishi hayo wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Natalia Bahati Kilangi ambaye hadi mauti yanamkuta, alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SAUT.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa salamu za Serikali kwenye mazishi hayo.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akitoa salamu za rambirambi kwenye mazishi hayo kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa wengine Tanzania.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akiwa na viongozi mbalimbali kwenye ibada ya kumuaga marehemu Natalia Bahati Kilangi ambaye alikuwa mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi.
 Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa tatu kulia) wakiwa kwenye ibada ya kumuaga marehemu Natalia Bahati Kilangi ambaye alikuwa mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi.
 Ndugu, jamaa, marafiki, viongozi mbalimbali pamoja na viongozi wa dini wakiwa kwenye mazishi hayo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.