LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maonesho ya Biashara Afrika Mashariki 2019 kutoa fursa zaidi kwa washiriki

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki ambayo huandaliwa kila mwaka na Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa Mwanza yanatarajia kuanza Agosti 30 hadi Septemba 08, 2019.

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa Mwanza, Dkt. Elibariki Mmari alisema maonesho hayo ya 14 yatafanyika katika viunga Rock City Mall yakiwa na kauli mbiu "kuongeza ubunifu katika uzalishaji na biashara katika kukuza uchumi wetu".

Dkt. Mmari alisema malengo ya maonesho hayo ni pamoja na kutoa fursa kwa jumuiya ya wafanyabiashara kuimarisha mtandao wa masoko na usambazaji wa bidhaa zao.

Alisema pia ni kutoa mchango wao kwa vitendo katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo 2025.

Katika maonesho yaliyofanyika mwaka jana 2018, zaidi ya wananchi laki mbili walitembelea maonesho hayo ambapo mategemeo kwa mwaka huu 2019 ni idadi kuongeza zaidi hadi kufikia laki tatu.
Imeandaliwa na Judith Ferdinand

No comments:

Powered by Blogger.