LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wamiliki na wafanyakazi wa vyombo vya usafiri majini wakumbushwa wajibu wao

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Picha kutoka maktaba ikimuonesha Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa kwenye usafiri wa boti ndani ya Ziwa Victoria akielekea wilayani Ukerewe.

Judith Ferdinand, BMG
Wamiliki na wafanyakazi wa vyombo vya usafiri majini wametakiwa kujenga utamaduni wa kutoa elimu ya usalama ikiwemo umuhimu wa kuvaa vifaa vya uokozi kama maboya kwa abiria wanaotumia vyombo vyao kabla ya kuanza safari.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Mfawidhi wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoa wa Mwanza, Patrick Mipawa na kuongeza kwamba uvaaji vifaa vya uokozi ikiwemo maboya ni muhimu kwa kila abiria anayetumia usafiri wa majini kwani husaidia kuokoa maisha pale inapotokea dharura/ ajali.

Pia amewataka watumiaji vyombo vya usafiri majini kuzingatia matumizi ya maboya mara tu wanapoingia katika vyombo hivyo ili kuokoa maisha endepo chombo kitapata hitilafu majini na kwamba TASAC imekua ikitoa elimu ya uvaaji maboya kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara pamoja na mtu mmoja mmoja hususani maeneo ya visiwani.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Polisi Wanamaji Mkoa wa Mwanza, Inspekta Wenceslaus Muchunguzi anasema TASAC na Polisi wamepewa jukumu la kusimamia masuala ya usafiri majini ikiwemo kuhimiza utumiaji wa maboya hivyo kabla ya kuingiza chombo ziwani lazima wakague kama kina vifaa hivyo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.