LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bloggers wapewa mafunzo kuhusu Maadili ya Uandishi wa Habari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mbadala (Alternative Media) nchini Tanzania vinavyojumuisha mitandao ya kijamii ikiwemo magazeti tando (Blogs) pamoja na luninga za mtandaoni (Online TV) wamekutana jijini Dodoma kwa ajili ya kupata mafunzo ya siku mbili kuanzia Agosti 22, 2019 kuhusu maadili ya uandishi wa habari ili kuwawezesha kufanya kazi kwa weledi.

Waandishi hao wapatao 25 ni wale wanaotekeleza mradi wa utetezi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu (Data Driven Advocacy-DDA) unatekelezwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Arusha (APC) kwa usimamizi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT Tanzania.
#BMGHabari
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Allan Lawa akiwasilisha mada kuhusu Maadili ya Uandishi wa Habari (Media Ethical Reportage/ Code of Ethics).
Picha na Kadama Malunde

No comments:

Powered by Blogger.