LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanahabari Kanda ya Ziwa wapewa mafunzo kuhusu habari za uchaguzi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

#BMGHabari
Wakati Tanzania ikielekea kwenye chaguzi mbalimbali, Mtandao wa asasi za kiraia zinazoangalia uchaguzi Tanzania (TACCEO) chini ya Kituo cha Sheria za Haki za Binadamu (LHRC), umetoa mafunzo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa ili kuwajengea uwezo kuandika habari za uchaguzi kwa weledi.

Mafunzo hayo ya siku tatu yalianza Agosti 22, 2019 jijini Mwanza yakishirikisha wanahabari kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kagera na Kigoma.

Mwakilishi kutoka LHRC ambaye pia ni Mratibu wa mafunzo hayo, Joseph matarajioni ni kuona wanahabari wakifanya kazi zao kwa weledi ikiwemo kuwahamasish wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, kuthubutu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kushiriki zoezi la kupiga kura.

Naye mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo, Wakili Gelina Fuko kutoka taasisi ya Tangible Initiatives for Local Development Tanzania (TIFLD)  aliwahimiza wanahabari kupaza sauti kwa ajili ya makundi ya watu maalum wakiwemo wenye ulemavu, wanawake na wazee ili washiriki ipasavyo kwenye chaguzi zijazo ukiwemo uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2019.

Nao washiriki waliahidi kuyatumia vyema mafunzo hayo ili kuongeza uelewa kwa wanajamii kutambua haki zao ikiwemo kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi pamoja na kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.
Mwakilishi kutoka kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Joseph Oleshaghai ambaye pia ni mratibu wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanahabari kuandika kwa weledi habari za uchaguzi.
Mkurugenzi wa taasisi ya Tangible Initiatives for Local Development Tanzania (TIFLD), Gelina Fuko akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mwakilishi wa BMG Online TV jijini Mwanza, Fedrick Chibuga akichangia mda kwenye mafunzo hayo.
Picha na Malunde Blog

No comments:

Powered by Blogger.