LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waandishi wa habari mitandaoni watakiwa kutimiza wajibu wao

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) vinavyohusisha mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Blogs na Luninga za Mtandaoni wametakiwa kutimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuandika kwa wingi habari za utetezi wa haki za binadamu.

Rai hiyo imetolewa Agosti 20, 2019 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Arusha, Claud Gwandu wakati akifungua mafunzo kuhusu haki za binadamu kwa waandishi wa habari wa mtandaoni nchini Tanzania wanaotekeleza mradi wa utetezi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu (Data Driven Advocacy-DDA).

"Haya ni mafunzo ya tatu mnapewa lakini bado hatujaona habari za haki za binadamu kwa wingi kama ambavyo tunatakiwa kufanya hivyo tutumie vyema fursa hii kutimiza wajibu wetu" Amesisitiza Gwandu.

Akiwasilisha mada kuhusu haki za binadamu, Mwezeshaji wa mafunzo hayo Wakili Froldius Mutungi amesema waandishi wa habari wana wajibu wa kupaza sauti kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa kwani hazipaswi kuminywa ama kutolewa na mtu yeyote kwani ni stahiki ya kila mwanadamu.

Mradi wa DDA kwa kundi namba tatu linalohusisha waandishi wa habari wa mitandaoni unatekelezwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari Mkoa Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani chini ya taasisi za Freedom House pamoja na PACT.
#BMGHabari
 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC), Claud Gwandu akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo
 Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Wakili Froldius Mutungi akiwasilisha mada kuhusu Haki za Binadamu kwenye mafunzo hayo.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini uwasilishaji wa mada kwenye mafunzo hayo.
Waandishi wa habari mtandaoni wanajengewa uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya utetezi wa haki za binadamu kwa muda wa siku nne kuanzia Agosti 20-23, 2019.
Picha na Malunde Blog & Gsengo Blog

No comments:

Powered by Blogger.