Taasisi ya APHFTA yatoa bilioni 1.4 kwa watoa huduma za afya mkoani Geita
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Chama cha
Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania (APHFTA) kupitia taasisi yake ya kifedha “Afya
Microfinance” kimetoa shilingi bilioni 1.4 kama mikopo kwa watoa huduma za afya
mkoani Geita ili kuboresha zaidi huduma zao.
Mkurugenzi
wa Miradi kutoka APHFTA, Elizabert Bonareri aliyasema hayo Agosti 26, 2019
wakati akielezea mafanikio ya utekelezaji wa mradi wa kupambana na Malaria
mkoani Geita katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Ni baada ya
wawakilishi kutoka taasisi za Comic Relief na GSK zinazofadhili mradi huo
kutembelea huduma mbalimbali zilizoboreshwa kupitia taasisi ya APHFTA ikiwemo Maabara,
Vituo vya Afya, Zahanati pamoja na Maduka ya Dawa Muhimu katika Mkoa wa Geita.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wawakilishi kutoka Comic Relief & GSK wakiwa kwenye moja ya duka la dawa muhimu mkoani Geita lililonufaika na mkopo kutoka APHFTA.
Taasisi ya APHFTA inahimiza watoa huduma za afya kuwa wanachama ili kunufaika na mikopo mbalimbali ili kuboresha huduma zao.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: