Shirika la KIVULINI lawezesha utekelezaji wa MTAKUWWA mkoani Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Shirika la
kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI limekabidhi kompyuta mpakato
(Laptops) 10 katika idara mbalimbali za Serikali mkoani Mwanza ili kuongeza
ufanisi wa utekelezaji mkakati wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watoto na
wanawake (MTAKUWWA).
Zoezi la
kukabidhi kompyta hizo zenye thamani ya shilingi milioni 12 limefanyika Agosti
27, 2019 kwenye mafunzo kwa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto na
Wanawake Mkoa Mwanza.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally amesema zitasaidia uwekaji
kumbukumbu na utoaji taarifa na tathmini ya utekelezaji wa MTAKUWWA huku pia
shirika hilo likiwa limesaidia uimarishaji mfumo wa utunzaji kumbukumbu (Data
Base) ngazi ya Mkoa Mwanza pamoja na Wilaya Misngwi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Dkt. Christopher Kadio akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa Kamati
ya Ulinzi na Usalama wa Watoto na Wanawake Mkoa Mwanza.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda (katikati) wakiwa meza kuu kufuatilia mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akisisitiza jambo kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo.
Tazama BMG Online TV hapa chimi
No comments: