LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ulega asisitiza Ushirika kulinda rasilimali za Uvuvi Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, BMG
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema uanzishwaji wa ushirika wa wavuvi utasaidia kulinda rasilimali za uvuvi nchini.

Ulega aliyasema hayo alipokutana na wadau wa vyama vya ushirika mkoani Mwanza wanaonufaika zaidi na rasilimali za uvuvi na kuongeza kwamba kupitia Ushirika wavuvi wataweza kulinda rasilimali za uvuvi.

"Lengo la Serikali ni kuona sekta ya uvuvi inakua na kuchangia pato la Taifa huku wavuvi wakiwa na maisha bora kwa kila mmoja kushiriki katika ulinzi wa rasilimali za uvuvi kwa mujibu wa sheria kupitia Ushirika ambapo pia watapata fursa ya kukopeshwa fedha na kupatiwa elimu kutoka taasisi za kifedha" alisema Ulega.

Naye Katibu wa Chama Kikuu Cha Ushirika wa Wavuvi Tanzania (Chakuwata), Bakari Kadabi alisema suala la Ushirika wamelipokea vyema na wanaamini ndio mwarobaini wa kutokomeza uvuvi haramu nchini ambapo alitumia fursa hiyo kuwahimiza wavuvi kuanzisha vyama vya Ushirika.

No comments:

Powered by Blogger.