LIVE STREAM ADS

Header Ads

NIDA yatoa rai kwa wananchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, BMG
Wananchi wametakiwa kuachana na tamaduni za kupuuzia vitu vya msingi vinavyotolewa na Serikali ikiwemo suala la uandikishaji wa vitambulisho vya taifa.

Hayo yalibainishwa na Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ( NIDA), Agnes Gerald wakati akizungumza katika maonesho ya 14 ya Afrika Mashariki yaliondaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) yanayofanyika jijini Mwanza kuanzia Agosti 30 hadi septemba 8 mwaka huu.

Alisema changamoto inayowakabili hususani katika zoezi la uandikishaji vitambulisho vya Taifa ni wananchi kutoitikia wito kwa wakati hivyo wanasubilia siku zinapoisha ndipo wanajitokeza kwa wingi huku wakihitaji kuhudumia kwa wakati huo.

Aidha aliwataka wananchi kujitokeza mapema katika maonesho hayo na kutembelea banda lao ili wapatiwe namba ya utambulisho na maombi yao yafanyiwe kazi kwa ufasaha ingawa wanayo huduma ya haraka hivyo kuwepo kwa huduma ya waombaji wa dharura isigeuke kuwa kigezo cha kusubili ama kujenga tamaduni wa kwenda dakika za mwisho na kulifanya jambo hilo kuwa kama zimamoto.

Kwa upande wake Msajili wa NIDA Mkoa wa Mwanza, Raphael Manase alisema jambo la msingi ni kutumia wasaa huo na kutoa taarifa za msingi zilizo sahihi na kufuata vigezo ili kupata kitambulisho.

Alisema kuna baadhi ya fomu zina mapungufu hivyo ni vyema utakapoona muda unapita bila kupata taarifa yoyote ama namba ya utambuzi ni vyema kufuatilia kwenye ofisi za NIDA zilizopo kila wilaya ama kwa watendaji wa vijiji kubaini nini tatizo na kutoa taarifa zilizo sahihi ili kuweza kushugulikiwa.

"Tatizo la wengine kupata vitambuliasho na wengine kukosa , wakati tunafanya uchakataji tumebaini baadhi ya fomu zinamapungufu hivyo ni vyema mtu kufatilia na kubaini tatizo na kushugulikiwa"alisema Manase.

No comments:

Powered by Blogger.