LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Ilala atuma salamu kwa wafanyabiashara wadogo soko la Buguruni

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Azmala Said, Dar
Mkuu wa Wilaya Ilala mkoani Dar es salaam, Sophia Mjema amewataka wafanyabiashara wadogo katika soko la Buguruni wanaofanyia biashara zao nje ya soko kwa kigezo cha kuwa na vitambulisho vya wajasiriamali kurejea mara moja ndani ya soko hilo.

Mjema alitoa agizo hilo Oktoba 30, 2019 alipofanya ziara sokoni hapo kufuatia malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Buguruni kuwalalamikia wenzao wanaofanyia biashara nje ya soko hilo.

"Kwa hili sitowasamehe, mnawaumiza wenzenu, kwa nini mkwepe ushuru wakati wenzenu wanipa, nataka mrudi ndani ya soko haraka na wasio taka tunawachukulia hatua" Alisisitiza  Mjema.

Aidha Mjema aliwaonya baadhi ya madalali wanaokiuka sheria za biashara kwa kuwanyonya wafanyabiashara sokoni hapo akionya kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Naye Mkurugenzi Manispaa Ilala, Jumanne Shauri alishauri kuwepo kwa mikataba maalum ya kisheria kati ya wafanyabiashara wa soko hilo na madalali ili kuhakikisha pande zote zinanufaika kibiashara.

No comments:

Powered by Blogger.