LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWAUWASA wapewa miezi miwili mradi wa maji wilayani Sengerema

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ametoa muda wa miezi miwili hadi kufikia Januari 2020 mradi wa maji Nyampande-Sengerema uwe umekamilika na kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli.

Mradi huo unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) unagharimu shilingi bilioni 1.8 ukitarajiwa kuhudumia zaidi wa wananchi elfu 10 wa Vijiji vya Kawekamo, Nyampande na Nyasenga wilayani Sengerema.

Mongella aliyasema hayo Oktoba 11, 2019 wakati akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea maelekezo ya ufumbuzi.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.