LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mila potofu ya kuongeza mvuto kwa mabinti yalalamikiwa mkoani Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mila potofu ya “samba” katika Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga imelalamikiwa kukwamisha juhudi za Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kupambana na mimba za utotoni wilayani humo.

Inaelezwa kwamba mila hiyo potofu inahusisha baadhi ya wazazi kuwapeleka mabinti zao kwa waganga wa kienyeji ili wapakwe dawa ya asili “samba” ili wawe na mvuto kwa wanaume hatua ambao inachochea ongezeko la mimba na ndoa za utotoni ambapo kwa mwaka 2017/19 kesi 101 za wanafunzi kubeba ujauzito ziliripotiwa polisi wilayani Kishapu.

Hayo yalielezwa Septemba 30, 2019 kwenye uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza aina zote za ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto Wilaya Kishapu inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI.

 Mkuu wa Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba akizindua kampeni hiyo alikemea baadhi ya wananchi wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia akisema Serikali haiwezi kuvumilia vitendo hivyo kuendelea wakati Taifa likielekea kwenye uchumi wa kati.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Baadhi ya wanafunzi na wazazi wakifuatilia kampeni hiyo.
 Uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia wilayani Kishapu.
 Baadhi ya wazazi na wanafunzi wakifuatili kampeni hiyo.
 Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wakifuatilia uzinduzi wa kampeni hiyo.
 Mkuu wa Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ambapo alikemea wananchi kujihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia akisema Serikali haiwezi kuvumilia vitendo hivyo kuendelea.
 Diwani wa Kata ya Talaga wilayani Kishapu akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo.
 Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana KIVULINI, Yassin Ally akitoa elimu kwa wanafunzi na wazazi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ikiwemo kusomesha watoto wao badala ya kushiriki imani potofu katika jamii.
 Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwa amepiga magoti kama ishara ya kutoa msisitizo kwa viongozi mbalimbali wilayani Kishapu kutimiza wajibu wao ili kupambana na ukatili wa kijinsia wilayani humo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.