LIVE STREAM ADS

Header Ads

PWANI "wananchi wajitokeza kwa wingi kusajili wa laini za simu kwa alama za vidole"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wananchi katika Chalinze mkoani Pwani wakiwa kwenye foleni kuitikia zoezi la usajili wa laini zao za simu kwa alama za vidole kupitia kupitia kampeni ya Mnada kwa Mnada inayoratibiwa na TCRA kwa lengo la kuhamasisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Na Chalila Kibunda, Pwani
Afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akitoa elimu kwa wananchi kupitia kampeni ya Mnada kwa Mnada inayohamasisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Wakazi wa Chalinze mkoani Pwani wamejitokeza kwa wingi kwenye kampeni ya Mnada kwa Mnada inayoratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na makampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Mkuu wa TCRA Kanda ya Mashariki, Mhandisi Lawi Odiero amesema kampeni hiyo inatoa fursa kwa wananchi kusajili laini za simu kwa alama za vidole na huduma nyinginezo kutokana na kuwepo kwa mnyororo wa wadau wote wa mawasiliano.

Mhandisi Odiero amewasihi wananchi kutumia kampeni hiyo ili kusajili laini za simu zao kabla muda wa miezi mitatu uliotolewa hadi kufikia Disemba 31, 2019 haujafikia ukomo na hivyo kuingia kwenye hati hati ya kukosa huduma ya mawasiliano.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA, Mabel Masasi amesema mwitikio wa wananchi kuhitaji vitambulisho vya NIDA ni mkubwa kwa ajili ya kusajili laini zao za simu kwa alama za vidole
  Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.