Mkandarasi afanikiwa kudhibiti mkondo wa maji “ghorofa lajengwa kwa kasi”
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkandarasi
kampuni ya Mzinga amefanikiwa
kudhibiti mkondo wa maji ya Ziwa Victoria yaliyokuwa yanakwamisha kasi ya ujenzi
wa jengo la ghoroma mbili kwa ajili ya wodi ya wanaume katika Hospitali ya
Wilaya Nyamagana “Butimba” mkoani Mwanza.
Serikali
ilitenga shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa wodi hiyo ulioanza mwaka
2017 kwa kusuasua kutokana na mkondo huo wa maji hatua iliyosababisha
mabadiliko ya mchoro kufanyika na hivyo Halmashauri ya Jiji la Mwanza kusimamia
gharama zilizoongezeka.
Mkuu wa Mkoa
Mwanza, John Mongella akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu
Tawala Mkoa Mwanza, Christopher Kadio pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba ametembelea ujenzi wa wodi hiyo inayotarajiwa
kukamilika mwishoni mwa mwezi Disemba, 2019.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini
Madiwani wa Jiji la Mwanza wakagua miradi mbalimbali ya maendeleo
#PamojaDaimaBMG
No comments: