LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ujenzi jengo la abiria uwanja wa ndege Mwanza “kazi ni usiku na mchana”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Ujenzi wa jengo jipya na la kisasa kwa ajili ya abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa Mwanza unaendelea kwa kasi huku msisitizo wa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ukiwa ni kukamilika ndani ya miezi sita badala ya miezi 12.

Itakumbukwa ujenzi wa jengo hilo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Julai 15, 2019 alipokuwa akizindua miradi ya afya katika Hospitali ya Rufaa Bugando ambapo aliagiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Manispaa ya Ilemela kuchangia gharama za ujenzi huo zinazokadiriwa kuwa Shilingi Bilioni nne.

Jengo hilo linalojengwa usiku na mchana na kampuni ya SUMA JKT kwa usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, litakapokamilika litakuwa na uwezio wa kuhudumia zaidi ya abiria 600 kwa wakati mmoja ambapo ujenzi ulianza rasmi Septemba 25, 2019.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.