Filimbi yapulizwa Tamasha la Urithi (Urithi Festival 2019) jijini Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ametembelea maonesho ya Tamasha la Urithi (Urithi Festival 2019) katika viunga vya Rock City Mall jijini Mwanza, lililoanza Oktoba 31, 2019 likitarajiwa kuhitimishwa Novemba 02, 2019 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Tamasha la Urithi 2019 kitaifa mkoani Mwanza linaandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Tamasha la Urithi 2019 kitaifa mkoani Mwanza linaandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Picha na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akicheza mchezo wa bao alipotembelea mabanda kwenye Tamasha la Urithi 2019 jijini Mwanza.
Tamasha la Urithi linalenga kuutangaza utamaduni wa Mtanzania pamoja na Vivutio mbalimbali vya Utalii.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwasili kwenye tamasha hilo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa Mwanza akisalimiana na maafisa mbalimbali alipotembelea banda la Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambalo ni mdhamini mkuu wa tamasha la Urithi 2019.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella wakifuatilia ngoma mbalimbali za asili kwenye tamasha hilo.
Viongozi wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Urithi 2019 jijini Mwanza wakifuatilia ngoma mbalimbali za asili.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) pamoja na viongozi mbalimbali wakifurahia burudani kwenye tamasha hilo.
Kijana huyu alikuwa kivutio kikubwa kwa uwezo wake wa kumeza vitu mbalimbali ikiwemo misumari, chupa na betri.
Kijana akikaguliwa kama kweli kameza betri....NI KWELI KAMEZA hahahahaaaaa ni ubunifu tu wa utamaduni wa Mtanzania.
Kilele cha Tamasha la Urithi ni Novemba 02, 2019 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Karibu Tamasha la Urithi wa Mtanzania katika viunga vya Rock City Mall jijini Mwanza, hakuna kiingilioni.
Mmoja wa wadau wakubwa wa Utalii mkoani Mwanza, Matia Levi akifuatilia tamasha hilo ambalo pia limesheheni burudani na bidhaa mbalimbali za asili.
Baada ya Tamasha la Urithi 2019 kufikia tamati Novemba 02, 2019 itafuatia safari ya kuelekea kwenye hifadhi ya Burigi Chato Novemba 03, 2019.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini
SOMA>>> Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa Mgeni Rasmi Tamasha la Urithi 2019 jijini Mwanza
SOMA>>> Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa Mgeni Rasmi Tamasha la Urithi 2019 jijini Mwanza
No comments: