LIVE STREAM ADS

Header Ads

Vijana wa Skauti wilayani Shinyanga wamuenzi Baba wa Taifa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Chama cha Skauti katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mjini kimeadhimisha kumbukizi ya miaka 20 tangu kifo cha Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Mnara wa Shule ya Msingi Bugoyi A ambapo siku anafariki dunia Mwenge wa Uhuru ulikuwa shuleni hapo. 

Maadhimisho hayo yalifanyika Oktoba 14, 2019 tarehe aliyofariki Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1999 akiwa nchini Uingereza akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas.

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga, Abubakari Hafeez Mkadamu aliwataka vijana hao wa Skauti kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo kwa kuwa wazalendo na kuipenda nchi yao pamoja na kudumisha amani na upendo. 

Alisema zawadi pekee ambayo vijana hao wanapaswa kumpatia Mwalimu Nyerere ni kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani ya nchi ambayo aliiacha Baba wa Taifa na siyo kumuenzi kwa kutenda mambo mabaya ikiwamo kujiingiza kwenye madawa ya kulevya. 

"Vijana ni Taifa la kesho hivyo nyie kama Skauti ambao mnapitia mafunzo mengi mnapaswa kwenda kueneza elimu kwa vijana wenzenu ya kuwa wazalendo na kuipenda nchi, pamoja na kudumisha amani na upendo vitu ambavyo ametuachia Baba yetu wa Taifa" Alisema Mkadamu na kuongeza;

"Pia nawaomba na wanafunzi kote nchi mumuenzi Baba yetu wa Taifa kwa kusoma kwa bidii na kumfukuza adui ujinga, moja ya maadui watatu aliokuwa akiwapinga na kuachana na tabia ya kwenda na simu mashuleni na kuanza kuchati na kuwasababishia kufanya vibaya kimasomo" aliongeza Mkadamu.

Naye Katibu wa Skauti Wilaya ya Shinyanga, Vicent Kanyogoto alisema wamedhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere kwenye mnara huo ambapo wamekaa muda wa siku nne akifanya shughuli za usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti na kuwapatia vijana elimu ya uzalendo pamoja na kudumisha amani na upendo. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga, Abubakari Hafeez Mkadamu akizungumza kwenye kwenye maadhimisho hayo. Vijana wa Skauti wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga, Abubakari Hafeez Mkadamu. Mjumbe wa Kamati ya Ufuatiliaji na Hamasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga, Eric Daudi akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo. Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ndembezi, Pendo John akitoa nasaha kwa vijana. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bugoyi A, Anna Alute akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo. Mwanafunzi Emmanuel Barnaba (kushoto) anayesoma Shule ya Msingi Bugoyi A akisoma risala ambapo aliiomba Serikali kuboresha miundo mbinu ya Shule hiyo ilikuendana na hadhi ya Mnara wa kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere. Katibu wa Chama cha Skauti Wilaya ya Shinyanga, Vicent Kanyogota akizungumza kwenye maaadhimisho hayo. Vijana wa Skauti wilayani Shinyanga. Vijana wa Skauti wilayani Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho hayo. Mafundi wakiendelea kujenga Mnara wa kumbukumbu wa Mwalimu Nyerere katika Shule ya Msingi Bugoyi A wilayani Shinyanga. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga, Abubakari Hafeez Mukadamu akipanda mti katika Shule ya Msingi Bugoyi A, mahali ulipo Mnara wa Mwalimu Nyerere. Kamishina wa Skauti Wilaya ya Shinyanga, Peter Mgalula akipanda mti. Katibu wa Skauti Wilaya ya Shinyanga, Vicent Kanyogoto akipanda mti katika eneo la Shule ya Msingi Bugoyi A. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bugoyi A, Anna Alute akipanda mti. Vijana wa Skauti nao wakipanda miti. Vijana wa Skauti wakijipanga kwa kufanya maandamano kuzunguka mjini Shinyanga huku wakiwa na picha ya Mwal. Julius Kambarage Nyerere. Vijana wa Skauti wakijiandaa kufanya maandamano huku wakiwa wamebeba picha ya Rais wa awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli. Vijana wa Skauti wakiwa kwenye maandamano ya amani kama ishara ya kumuenzi Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Maandamano yakiendelea. Maandamano na burudani. Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga akivalishwa skafu baada ya kuwasili kwenye Mnara wa Mwalimu Nyerere katika Shule ya Msingi Bugoyi A. Skauti wakitoa burudani. Vijana kutoka kundi la The Fire mjini Shinyanga nao wakitoa burudani. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga, Abubakari Hafeez Mkadamu akihitimisha maadhimisho hayo kwa kugawa vyeti kwa vijana waliohitimu mafunzo ya Skauti. Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea. Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea. Zoezi la ugawaji vyeti. Skauti wilayani Shinyanga na viongozi wao wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Shinyanga, Neema Mkanga (katikati mwenye kilemba kichwani).
Imeandaliwa na Marco Maduhu, Malunde 1 Blog

No comments:

Powered by Blogger.