LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Ilemela aunga mkono ujenzi wa Kanisa la EAGT Kahama

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Afisa Tarafa wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Godfrey Mzava akizungumza katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la EAGT Kahama wilayani humo kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula.
Judith Ferdinand, Mwanza
 Mchungaji wa Kanisa la EAGT Kahama wilayani Ilemela, Festo Kwindeka akizungumzia harambee ya ujenzi wa kanisa hilo.
 Baadhi ya waumini wa Kanisa la EAGT Kahama wilayani Ilemela wakifuatilia harambee hiyo.
Watoto wa Kanisa la EAGT Kahama wilayani Ilemela wakiimba katika harambee hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Dkt. Angeline Mabula ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema Serikali inatambua mchango wa taasisi za dini nchini katika kuwaletea wananchi maendeleo hivyo itaendelea kushirikiana na taasisi hizo.

Afisa Tarafa wa Wilaya ya Ilemela, Godfrey Mzava alitoa kauli hiyo kwa niaba ya mbunge huyo wakati akizungumza kwenye harambee ya ujenzi wa Kanisa la EAGT Kahama lililopo Kata ya Kahama wilayani Ilemela.

Alisema Serikali inatambua michango ya taasisi za kidini kwa jamii ikiwemo utoaji wa elimu, huduma za afya na kiroho zinazosaidia kuchochea amani, upendo na kupunguza matendo yasiyo faa katika nchi.

"Serikali inatambua mchango wenu katika kuleta maendeleo, niwahakikishie ushirikiano kwa jambo lolote lile mtakaloona linamanufaa kwa watu wetu, Mbunge wa Jimbo la Ilemela yuko pamoja na waumini wa Kanisa hili katika kuhakikisha hatua ya ujenzi ilipofikia inakamilika, ataanza kwa kutoa matofali 800" alisema Mzava.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la EAGT Kahama, Festo Kwideka alisema lilianza na waumini watano na mpaka sasa lina waumini 100 na kwamba lilikuwa na changamoto ya eneo la kuabudu hususani msimu wa mvua na hivyo kuamua kuanza ujenzi wa jengo la kisasa kwa ajili ya ibada.

Akisoma risala kuhusu ujenzi wa Kanisa hilo, Dorice Merengo alisema ujenzi huo bado unahitaji vifaa mbalimbali ikiwemo nondo, saruji, bati, mbao na misumari na hivyo kuwaomba wadau wengine kuunga mkono jitihada zilizopo ili kukamilisha ujenzi kwa wakati.

No comments:

Powered by Blogger.