LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwanza watakiwa kununua simu za kupokea taarifa za hali ya hewa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ameagiza hadi kufikia Disemba 01, 2019 idara za uvuvi na kilimo katika Halmashauri zote kuhakikisha zinakuwa na simu maalum kwa ajili ya kupokea taarifa za hali ya hewa na kuzifikisha kwa wananchi.

Mongella alitoa agizo hilo Novemba 06, 2019 wakati akifungua warsha ya utoaji wa elimu kuhusiana na  huduma za hali ya hewa zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) iliyoshirikisha viongozi mbalimbali wakiwemo wavuvi kutoka wilaya za Sengerema (Mwanza) na Mulema (Kagera).
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akitoa taarifa kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa kuboresha Huduma za Hali ya Hewa katika Bara la Afrika unaojikita kutoa elimu kwa wavuvi kuhusiana na huduma za hali ya hewa.
 Washiriki kutoka Sengerema mkoani Mwanza pamoja na Muleba mkoani Kagera wakifuatilia warsha hiyo kuhusu utoaji wa elimu kuhusiana na  huduma za hali ya hewa zitolewazo na TMA zinazozingatia athari.
 Washiriki wakiwa kwenye warsha hiyo.
 Kikundi cha ngoma asili ya kabila la wasukuma Bujora kikitoa elimu kwa njia ya nyimbo kuhusu umuhimu wa taarifa za hali ya hewa kwa wavuvi.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.