Machinga jijini Mwanza wawakingia kifua wateule wa Rais "tusichonganishwe"
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Muungano wa Machinga Mkoa Mwanza
umesema hakuna mgogoro wowote baina yao na wateule wa Rais kufuatia agizo la
kuwaondoa baadhi ya wafanyabiashara wakubwa waliokuwa katika eneo la Pamba kwa
kigezo kwamba nao ni machinga.
Wafanyabishara hao walijenga makontena
katika eneo hilo baada ya kupisha mradi wa ujenzi wa soko kuu jijini Mwanza kwa
kigezo kwamba nao ni machinga hatua ambao ilipingwa vikali na viongozi wa
machinga wakisema hizo ni mbinu za ukwepaji kodi na kwamba machinga waliopisha
mradi huo tayari wamehamia eneo la Mitimirefu.
#BMGHabari
Mmoja wa machinga jijini Mwanza akizungumza na BMG.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini
No comments: