LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Viti Maalum Njombe (CCM) ahitimisha ziara yake

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM Mkoa Njombe, Neema Mgaya amehitimisha ziara ya kikazi mkoani humo kwa kuunga mkono jitihada za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika ziara hiyo, Mgaya alitoa mifuko 150 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili (Tsh. 2,250,000) itakayoelekezwa kwenye miradi kadhaa ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba ya waalimu katika Shule ya Sekondari Ludewa pamoja na Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Kata ya lyamkena.

Pia miradi mingine ni ujenzi wa Zahanati ya Utengule, Ofisi ya Kijiji cha Ngamanga, Zahanati ya Kanisa Katoliki Mtwango pamoja na ujenzi wa  Kanisa la Pentekoste Igwachanya.

Mgaya alibainisha kwamba miradi mingine itakayonufaika na gawio la mifuko hiyo kuwa ni Shule ya Sekondari Usuka, Ofisi ya Serikali ya Kata Wanging'ombe pamoja na ile ya Kata ya Uhenga.

Katika hatua nyingine Mgaya pia alisaidia upatikanaji wa bendera za CCM kwa ajili ya nyumba 100 za mabalozi zenye thamani ya shilingi laki tatu (Tsh. 300,000).

"Pia nimekabidhi friji 15 za kampuni ya Cocacola kwa wafanyabiashara wa vinywaji baridi Njombe na kuwatembelea akina mama wajane katika Kata ya Utengule ambapo nimewachangia shilingi laki moja (Tsh. 100,000) ili kuunga mkono jitihada zao za kujiletea maendeleo" alibainisha Mgaya.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa Njombe, Neema Mgaya akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa baadhi ya watu wenye uhitaji mkoani humo.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa Njombe, Neema Mgaya (kulia) akikabidhi bendera za CCM kwa ajili ya mabalozi 
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa Njombe, Neema Mgaya (katikati) akikabidhi friji kwa wafanyabiashara mkoani humo. 
#BMGHabari

No comments:

Powered by Blogger.