LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shule ya Orkeeswa ya jijini Arusha yang'ara michezo ya Shule za Kimataifa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Ndajiri Lonyori kutoka shule ya Sekondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mchezo wa mpira wa kikapu wa wasichana chini ya miaka 19 wakati wa wikiendi ya michezo kwa Shule za kimataifa iliyofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro wikiendi iliyopita.

Shule ya Sekondary Orkeeswa kutoka mkoani Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali.
#BMGHabari
Ndajiri Lonyori kutoka shule ya Sekondari Orkeeswa akionesha kombe lao la ushindi wa mchezo wa Netball chini ya miaka 15 wakati wa Wikiendi ya Michezo kwa Shule za Kimataifa iliyofanyika Mjini Moshi.
Amani Isaya kutoka Shule ya Sekondari Orkeeswa akionesha kombe lao la ushindi wa mchezo wa Volleyball chini ya miaka 19.
Emmanuel Meibuko ambaye ni golikipa wa timu ya Shule ya Sekondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mpira wa miguu wa wavulana chini ya miaka 19 baada ya kuibuka washindi kwa goli 3-2 katika mechi iliyokuwa na ushindani mkali.

Shule ya Sekondari Orkeeswa iliyopo mkoani Arusha imeibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali ya Shule za Kimataifa iliyifanyika mkoani Kilimanjaro wikendi iliyopita.

Mashindano hayo yalishirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa kikapu, mpira wa miguu, tennis, swimmings, netball, volleyball, frisbie na rugby.

Timu za kikapu chini ya umri wa miaka 19 wasichana na wavulana wa umri huo pia zilionekana kuwa imara zaidi baada ya kuzishinda kwa kishindo timu za Shule nyingine.

Shule za kimataifa nchini zilikuwa na mashindano ya Wikiendi ya Michezo iliyoanza mwishoni Ijumaa Novemba 22, 2019 na kufikita tamati Jumapili Novemba 24, 2019

No comments:

Powered by Blogger.