LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko aweka jiwe la msingi ujenzi wa madarasa Bukombe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mbunge wa jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na ofisi ya waalimu katika Shule ya Msingi Mwalo iliyopo Kata ya Ushirombo jimboni humo.


Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini alifanya shughuli hiyo Novemba 25, 2019 ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Kata mbalimbali jimboni Bukombe yenye lengo la kukagua na kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Baadhi ya wakazi wa Ushirombo wakiunga mkono hoja za Mbunge wao Doto Biteko (hayuko pichani) alipokuwa akizungumza nao.
Diwani wa Kata ya Ushirombo, Lameck Warangi akitoa salamu zake baada ya mbunge wa Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini kufanya ziara katika Kata hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Ushirombo wakimlaki Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini 
Mapokezi ya Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini katika Kata ya Ushirombo.
Burudani katika Kata ya Ushirombo.
Sehemu ya mwonekano wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Mwalo wilayani Bukombe.
Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini akizungumza na wakazi wa Kata ya Ng'anzo alipofanya ziara katika kata hiyo.
Wakazi wa Ng'anzo wakimsikiliza Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini.
Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini alipofika kukagua ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Segwe Kata ya Ng'anzo.
Mwonekano wa choo ambacho kiko katika hatua ya mwisho kukamilika Shule ya Msingi Segwe.
Mwonekano wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Segwe baada ya kupauliwa.
Tazama BMG TV Online hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.