LIVE STREAM ADS

Header Ads

Meya Manispaa ya Ilemela awageukia wananchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, Mwanza
Wazazi na walezi katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wamehimizwa kutambua umuhimu wa elimu na hivyo kuhakikisha watoto wao wanakwenda shule huku pia wakitimiza wajibu wa kushiriki kuboresha miundombinu ya elimu.

Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Renatus Mulunga alitoa rai hiyo Novemba 08, 2019 kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kilicholenga kujadili taarifa za robo ya kwanza ya mwaka 2019/20

"Ni wajibu wa wazazi kuhamasisha wanafunzi kusoma ili kuwa na Taifa bora huku wananchi wakihakikisha miundombinu ya kusomea inaboreshwa na kukidhi mahitaji kwa kutatua changamoto ya upungufu wa madarasa" alisema Mulunga.

Naye Daniel Batare akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela alisema Halmashauri hiyo katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu imeshika nafasi ya kwanza kimkoa na ya pili kitaifa hivyo juhudi za kuboresha miundombinu ya elimu zitachochea matokeo mazuri zaidi kwa wanafunzi.

Hata hivyo mmoja wa wakazi wa Ilemela Francis Shukuru alisema Halmashauri kwa kushirikiana na Serikali kuu inapaswa kuja na mkakati wa muda mrefu ambao utasaidia upatukanaji wa madarasa, madawati pamoja na miundombinu mingine kuliko kila mwaka wananchi kuhimizwa kuchangia changamoto hizo.

No comments:

Powered by Blogger.