LIVE STREAM ADS

Header Ads

Viongozi wapya Misungwi waapishwa "kuwashughulikia watakaowakwamisha"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Viongozi wapya wa Serikali za Vitongoji na Vijiji katika Wilaya Misungwi mkoani Mwanza wakiambishwa kwa ajili ya kuanza rasmi kutimiza majukumu yao ya kiofisi huku wakitakiwa kuwashughulikia wale wote watakaojaribu kukwamisha jitihada zao za kuwatumikia wananchi.


Zoezi la kuwaapisha viongozi hao lilifanyika Novemba 28, 2019 ambapo Vitongoji 724 na Vijiji 114 wilayani Misungwi walipita bila kupingwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi uliofanyika Novemba 24, 2019.
#BMGHabari
 Viongozi wa Vitongoji na Vijiji wilayani Misungwi wakila kiapo.
 Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya Misungwi, Mhe. Esther Marick akitoa nasaha zake kwa viongozi hao kabla ya kuwaongoza kula kiapo cha utumishi. Wengine ni Mkuu wa Wilaya Misungwi Juma Sweda (kulia), Katibu Tawala Wilaya Misungwi (kushoto) pamoja na Msaidizi wa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Misungwi (wa pili kulia).
 Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Kisena Mabuba akitoa salamu zake kabla ya kuapishwa kwa viongozi wapya wa Vitongoji na Vijiji katika Halmashauri hiyo.
 Viongozi wapiya wilayani Misungwi kutoka Kata za Mamaye, Misungwi, Igokelo, Koromije, Mondo, Mwaniko pamoja na Mabuki wakiwa kwenye zoezi la kuapishwa.
 Baadhi ya viongozi wa Vitongoji na Vijiji wilayani Misungwi.
 Viongozi wapya wilayani Misungwi wakiwa kwenye zoezi la kuaoishwa kwa ajili ya kuanza majukumu yao.
 Viongozi hao wakijaza fomu za kiapo.
 Viongozi wapya wilayani Misungwi wakijaza fomu za kiapo.
 Wanawake pia walishiriki ipasavyo kuwania nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Vitongoji, Vijiji na Mitaa uliofanyika Novemba 24, 2019 nchini.
 Viongozi hao wakijaza fomu za kiapo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.