LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Mkuu Shirika la IRISH AID azindua makazi ya wananchi wilayani Misungwi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ireland (IRISH Aid) nchini Tanzania, Adrian FitzGerald amefanya uzinduzi rasmi wa makazi/ nyumba zinazoendelea kujengwa na wakazi wa Wilaya Misungwi mkoani Mwanza baada ya kupewa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia na kushirikiana katika kujiletea maendeleo.

Elimu hiyo imekuwa ikitolea na Halmashauri ya Wilaya Misungwi kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana KIVULINI ikiwa ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo mpango mkakati wa kitaifa wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA) kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.
#BMGHabari
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya Naibu Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ireland (IRISH Aid) nchini Tanzania, Adrian FitzGerald  kuzindua nyumba ya mmoja wa wakazi wa Misungwi.
 Wakazi wa Misungwi wakimsimika uchifu Naibu Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ireland (IRISH Aid) nchini Tanzania, Adrian FitzGerald ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa shirika hilo katika kuchochea maendeleo wilayani humo.
 Wakazi wa Misungwi wakiwa kwenye maandamano ya amani ya kuhamasisha maendeleo na kupinga ukatili wa kijinsia.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.