TANZANIA "bilioni 179 kutekeleza mradi wa Ujazilizi katika mikoa tisa"
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Waziri
wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo imetenga shilingi bilioni 179 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Ujazilizi
katika mikoa tisa nchini ukiwemo Mwanza kuanzia mwezi Januari 2020.
Mgalu aliyasema
hayo Disemba 22, 2019 wakati akijibu malalamiko ya wakazi wa Kata ya Kayenze iliyopo
Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza waliolalamika kutofikiwa na nishati ya umeme
kupitia mradi wa REA.
Aidha Mgalu ambaye
pamoja na shughuli nyingine aliwasha umeme katika maeneo mbalimbali ikiwemo
Shule ya Msingi Lutongo, alibainisha kwamba mradi huo wa Ujazilizi utafikisha umeme
katika maeneo yote ambayo hayakufikiwa na nishati hiyo kupitia mradi wa REA.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: