LIVE STREAM ADS

Header Ads

Viongozi wapya wilayani Ilemela wapewa angalizo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, Mwanza
Viongozi wapya kutoka Mitaa 171 ya Kata 19 za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkaoni Mwanza wakiwemo Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wametakiwa kuzingatia maadili, sheria na viapo walivyo vya kazi katika kutekeleza majukumu yao.

Akizungumza  wakati wa zoezi la kuwaapisha viongozi wapya wa Serikali za Mitaa, Hakimu wa Wilaya ya Ilemela Amani Sumari alisema viongozi hao wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria bila ya upendeleo na kuzingatia viapo vyao kwani watakaoenda kinyume watachukuliwa hatua za kisheria.

Naye Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga aliwataka viongozi hao kuendelea kushirikiana katika shughuli za kuleta maendeleo katika jamii huku wakizingatia uadilifu pamoja na kutenda haki kwa wananchi.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Shukrani Kyando alisema wenyeviti hao wakawe makini na matumizi ya mihuri hususani katika suala la ardhi ili kuepuka migogoro.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula ambaye pia Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwataka viongozi hao wapya kuzingatia utaratibu wa utoaji taarifa ya mapato na matumizi kwa wananchi.

"Nendeni mkawe daraja la kuwaunganisha watu na siyo kuwa ukuta wa kuwatenganisha, mkawatumikie watu na msiende kuwahusudu wenye fedha kwa kuhakikisha mnakuwa mbali na matumizi mabaya ya mihuri" alisisitiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.