LIVE STREAM ADS

Header Ads

Sababu za Aston Villa kumsajili Samatta

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Usakaji wa mshambuliaji katika klabu ya Aston Villa ulikuwa mgumu hali ya kwamba mkufunzi wa klabu hiyo Dean Smith alilazimika kukubali kwamba jeraha la mshambuliaji wa pekee Wesly lilikuwa limemaliza msimu wa mchezaji huyo hivyobasi shinikizo ya kutafuta mchezaji atakayechukua nafasi yake ilifaa kuanza.

Kulingana na mtandao wa Birmingham Live ulionukuliwa na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, wakati mmoja Villa ilishiriki mechi bila mshambuliaji mwafaka katika mechi za ligi na zile za kuwania makombe.

Ni hapa ambapo jina la Mbwana Samatta lilichipuka kama mshambuliaji ambaye angefunga magoli yaliohitajika na Villa ili kuweza kusalia katika ligi ya premia. Huku dau la £8.5m likikubalika ili kumnunua mchezaji huyo, hii ilikuwa bei ya chini ukitazama thamani ya washambuliaji kipindi hiki hususan wakati wa dirisha dogo la uhamisho la mwezi Januari ambapo wengi hawataki kuondoka katika klabu zao.

Lakini kwanini maskauti wa klabu ya Villa walifikiria kuhusu Mbwana Samatta kama mtu ambaye angeleta mafanikio na kuisaidia Villa kusalia katika Ligi.

Ripoti moja inasema kwamba , Samatta ambaya kwa sasa ana umri wa miaka 27 anaelekea kilele chake , huku akionekana kuwa na mchango mkubwa wa kuisaidia Villa kusalia katika ligi.

Mchezaji huyo mwenye urefu wa futi 5 ana uwezo wa kucheza kwa kutumia maguu yote mawili , ana kasi na kwamba ameimarika sana katika kipndi cha miaka miwili iliopita.

Amecheza mara 28 katika mashindano yote kufikia sasa msimu huu , akifunga mara 10 na kutoa pasi mbili zilizozsababisha magoli.

Mwaka uliopita alicheza mara 51 na kufunga magoi 32 mbali na kutoa pasi sita zilizosababisha magoli - hatua iliomfanya kushinda taji la mfungaji bora.

Ripoti ya watafutaji wa wachezaji katika klabu hiyo pia ilionyesha kwamba , Samatta ni aina ya mchezaji ambaye yuko tayari kufunga katika lango la upinzani.

Walidai kwamba Samatta ndio mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa katika ligi ya Ubelgiji kwa sasa , akiwa na sifa ambayo ni vigumu kwa upinzani kumzuia. Kulingana na The Citizen Tanzania Ripoti hiyo inasema kwamba Samatta ni mchezaji hatari anapopewa fursa ya kufunga na kuchangia magoli ndani na nje ya lango la upinzani.

Ana uwezo wa kufunga kwa njia tofauti. Uwezo wake wa kuruka angani ndio silaha yake kubwa hatua iliowafanya mabeki wa Liverpool akiwemo Vigil Van Dijk kushindwa kumkabili. Amefunga magoli matatu kupitia kichwa msimu huu rekodi iliopitwa na mchezaji mmoja pekee.

Msimu uliopita alifunga jumla ya magoli saba kupitia kichwa na rekodi hiyo ilipitwa na mchezaji mmoja pekee aliyefunga magoli manane.

Uwezo wake wa kuruka juu utaisaidia sana timu ya Smith wakati wa mipira ya adhabu mbali na kwamba umbo lake linamruhusu kuzuia mipira kabla ya kutoa pasi, ijapokuwa ni mahiri sana wa kumaliza anapopata pasi murua karibu na lango la upinzani.

Ilipendekezwa kwamba wakati Wesley atakaporudi, uwezekano wa yeye kushirikiana na Samatta utawaburudisha mashabiki wa Aston Villa iwapo kocha huyo atawachezesha pamoja.

Wote wana nguvu na uwezo wa kuwakabili mabeki hatua ambayo itatoa fursa kwa Jack Grealish na wengine kuonesha umahiri wao.
Imeandaliwa na BBC Swahili

No comments:

Powered by Blogger.