LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi wamlilia Rais Magufuli “kuzimwa laini za simu”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Wananchi mkoani Mwanza wamemuomba Rais Dkt. John Magufuli kuwaongezea tena muda wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ili wakamilishe zoezi la kupata nambari za vitambulisho vya uraia (NIDA).

Walitoa ombi hilo mbele ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aliyetembelea ofisi za NIDA Wilaya Nyamagana baada ya kupokea malalamiko kuhusu kusuasua kwa zoezi la uandikishaji katika ofisi hizo.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), laini za simu ambazo zilikuwa hazijasajiliwa kwa alama za vidole hadi Disemba 31, 2019 zingezimwa lakini Rais Dkt. Magufuli aliongeza muda hadi kufikia Januari 20, 2020.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.