LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mvua zazua balaa Mwanza "abiria wabebwa mgongoni kupanda feri"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimesababisha kina cha maji katika Ziwa Victoria kujaa na hivyo kuathiri magati ya kuegeshea kivuko (Ferry) cha MV. Tegemeo katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema. Pia miundombinu ya barabara ikiwemo madaraja imekatika na hivyo kuleta adha kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella Februari 06, 2020 alifanya ziara ya kukagua athari zilizotokana na mvua na kuagiza mamlaka za TEMESA, TANROADS pamoja na TARURA kushughulikia athari hizo haraka iwezekanavyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali kukagua athari za mvua katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema.
Juhudi za kurejesha mawasiliano ya moja ya daraja lililokatika kutokana na mvua katika Halmashauri ya Buchosa zikiendelea.
Mwonekano wa moja ya daraja lililokatika wilayani Sengerema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Hali hii imesababisha adha ya usafiri kwa wananchi wilayani Sengerema.
Juhudi za kurejesha huduma ya mawasiliano ya daraja lililokatika katika Halmashauri ya Buchosa zikiendelea.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.