LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jaji aonya ucheleweshwaji wa mashauri

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Sam Rumanyika amewata watendaji na wadau wa Mahakama kuepuka ucheleweshwaji wa mashauri usio wa lazima kwa kuwa hatua hiyo inaweza kukwamisha maendeleo kwa Taifa.

Jaji Rumanyika aliyasema hayo Februari 06, 2020 jijini Mwanza wakati akizungumza kwenye kilele cha Wiki ya Sheria nchini iliyofanyika ngazi ya Mkoa Mwanza katika viunga vya Mahakama hiyo.

Naye Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alisema mchango wa Mahakama katika kuchochea utulimu na amani umesaidia ukuaji wa ongezeko la pato la Mkoa Mwanza kutoka Tirioni 10.05 mwaka 2016 hadi Tirioni 12.6 mwaka 2018 na kuufanya Mkoa kushika nafasi ya pili baada ya Dar es salaam.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo.
 Wanahabari wakinasa matukio kwenye maadhimisho hayo.
 Viongozi mbalimbali wa Serikali na Mahakama wakifuatilia maadhimisho hayo.
  Viongozi mbalimbali wa Serikali na Mahakama wakifuatilia maadhimisho hayo.
 Baadhi ya Mawakili wa Serikali na Binafsi wakifuatilia maadhimisho hayo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.