LIVE STREAM ADS

Header Ads

STAMICO wakabidhiwa hati “kufanya uwekezaji mkubwa Mwanza”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limekabidhiwa rasmi hati ya umiliki wa ardhi kwa ajili ya kuanzisha mradi mkubwa wa kusafisha dhahabu (Gold Refinery) katika eneo mojawapo la viwanja vya kilichokuwa kiwanda cha ngozi (Mwanza Tanneries) jijini Mwanza. Makabidhiano hayo yalishuhudiwa Februari 05, 2020 na Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ofisini kwake.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) akimkabidhi Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Ziwa, Makwasa Biswalo hati ya umiliki wa ardhi kwa ajili ya kuikamidhi kwa mwakilishi wa STAMICO.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Ziwa, Makwasa Biswalo (wa tatu kushoto) akimkabidhi hati ya umiliki wa ardhi Mkurugenzi wa Raslimali Watu na Utawala wa STAMICO, Deusdedith Magala kwa ajili ya kuanzisha mradi wa kusafisha dhahabu.
Mkurugenzi wa Raslimali Watu na Utawala wa STAMICO, Deusdedith Magala (wa pili kushoto) akimshukuru Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kulia) baada ya kupokea hati ya umiliki wa ardhi kwa ajili ya shirika hilo kuanzia mradi wa kusafisha dhahabu.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.