LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wahandisi wasio na leseni wapigwa STOP Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amesema Wahandisi wasio na leseni hawatakuwa na sifa ya kufanya kazi mkoani Mwanza huku akiwataka wale waliosajiliwa kuhakikisha wanafufua leseni zao kwa wakati kila zinapofikia mwisho.


Mongella aliyasema hayo Februari 05, 2020 jijini Mwanza wakati akifunga warsha ya kuwajengea uwezo Wahandishi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa iliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (ERB) ikiambatana na zoezi la kuwaapisha na kuwakabiodhi leseni Wahandisi zaidi ya 40 baada ya kukidhi vigezo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akihitimisha warsha kwa Wahandisi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa iliyofanyika jijini Mwanza ikiambatana na zoezi la kukabidhi leseni kwa Wahandisi zaidi ya 40.
Msajili wa Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Mhandisi Patrick Barozi akizungumza kwenye warsha hiyo.
Wahandisi zaidi ya 40 wakila kiapo kabla ya kukabidhiwa leseni baada ya kuhitimu mafunzo yao.
Msajili wa Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Mhandisi Patrick Barozi (kulia) akisisitiza umuhimu wa Wahandisi kuwa na leseni. Kushoto ni Hakimu Mkazi Mahakama ya Mkoa Mwanza, John Jagadi aliyewaapisha Wahandisi kwenye warsha hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akimkabidhi leseni mmoja wa Wahandisi waliohitimu mafunzo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akimkabidhi leseni mmoja wa Wahandisi waliohitimu mafunzo.
Mhandisi wa Maji Wilaya Kwimba (kushoto) akipokea leseni yake kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia).
Wahandisi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa walioshiriki warsha hiyo.
Sekretarieti ikitekeleza majukumu yake kwenye warsha hiyo.
Maada ya warsha hiyo, wahandisi walitembelea ujenzi wa meli mpya ndani ya Ziwa Victoria pamoja na ukarabati wa meli ya MV. Victoria katika eneo la Bandari ya Mwanza Kusini ili kujifunza utekelezaji wa miradi hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.