LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mongella awaagiza Wakuu wa Wilaya kuwajibika

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amewataka Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala kushirikiana vyema na vyombo vya utoaji haki ikiwemo Mahakama ili kuhakikisha maamuzi yanayotolewa yanazingatia haki na kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.

Mongella aliyasema hayo Februari 04, 2020 wakati akifungua kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za Maadili ngazi za Wilaya na Mkoa kilichowajumuisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya pamoja na Watendaji wa Mahakama mkoani Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye kikao kazi cha kujadili muundo na utendaji kazi wa Kamati za Maadili ngazi za Wilaya na Mkoa kilichowahusisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya pamoja na Watendaji wa Mahakama mkoani Mwaza.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Joachim Tiganga akiwasilisha mada kuhusu muundo na utendaji Kamati za Maadili ya Mahakama ngazi za Wilaya na Mkoa.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.