LIVE STREAM ADS

Header Ads

Hospitali ya Bugando yaanza safari ya ujenzi wa Kituo cha Saratani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando iliyopo jijini Mwanza imeanza safari ya ujenzi wa Kituo/ Wodi ya kisasa kwa ajili ya kuboresha zaidi huduma ya matibabu ya ugonjwa wa Saratani hospitalini hapo.

Safari hiyo imeanza rasmi Februari 04, 2020 kwa Hospitali ya Bugando kuandaa harambee kwa ajili ya wadau kushiriki upatikanaji wa fedha za ujenzi wa wodi hiyo ambapo shilingi milioni 92.6 zilipatikana ikiwa ahadi ni milioni 97.4, hundi shilingi milioni 7.4 na taslimu shilingi milioni 6.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akizungumza kwa niabara ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kwenye harambee ya uchangiaji fedha kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa wodi ya saratani katika Hospitali ya Bugando.
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Renatus Nkwande akitoa salamu zake kwenye harambee hiyo.
 Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (ke) akiongoza harambee hiyo.
 Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (kushoto) akitoa pongezi kwa mmoja wa wadau walioshiriki harambee hiyo.
 Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (katikati) akiongoza harambee hiyo.
 Sehemu ya wshiriki wa harambee hiyo iliyofanyika ukumbi wa Rock City Mall Februari 04, 2020 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.