LIVE STREAM ADS

Header Ads

Abiria Kivuko cha MV. Tegemeo wakumbana na wakati mgumu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Abiria wanaotegemea Kivuko cha MV. Tegemeo kufanya safari zao kati ya Kaunda-Maisome-Kanoni katika Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema wanalazimika kubebwa mgongoni ama kukanyaga majini ili kuingia na kutoka ndani ya kivuko hicho baada ya kina cha maji ya Ziwa Victoria kuongezeka na kufunika magati.

Hali hiyo imewalazimu wakazi wa Halmashauri ya Buchosa kupaza sauti zao na kuomba Serikali kuwaondolea adha hiyo kwa kuwaboreshea magati hayo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amefika katika magati hayo na kushuhudia hali ikiwa si shwari na kuagiza TEMESA kutafuta ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
 Hali hii imetajwa kuhatarisha maisha ya abiria wanaotegemea usafiri wa Kivuko cha MV. Tegemeo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.