LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Ilala awapongeza viongozi wa dini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es salaam, Sophia Mjema amewapongeza viongozi wa dini nchini ambao kupitia huduma zao wanaendelea kuliombea mema Taifa huku wakijitenga na uchochezi wa kidini.

Mjema aliyasema hayo wakati akizungumza katika Kanisa la TAG lililopo Amana jijini Dar es salaam huku akiwahimiza viongozi wa dini kuendelea kuwa waamini katika kuliombea Taifa hususani mwaka huu 2020 ambao ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu.
Aidha Mjema aliwapongeza waumini wa Kanisa hilo kwa kujitoa kuliombea Taifa katika kipindic cha mwezi mzima kuanzia Januari 02 hadi 31, 2020.

Aliongeza kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuwakomboa wananchi kiuchumi kwa kila Halmashauri nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake ili kuwakopesha akina mama, vijana na wenye ulemavu.
Askofu wa Kanisa hilo, Lawrence Kameta alitoa pongezi kwa DC Mjema kwa namna anavyoshirikiana na viongozi wa dini mbalimbali bila ubaguzi na kwamba hatua hiyo inaendelea kuimarisha amani na mshikamano nchini.
Na Azmala Said, Dar

No comments:

Powered by Blogger.