LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la Umeme TANESCO latoa elimu kwa Wenyeviti wa Mitaa jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa Mwanza limetoa elimu kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa jijini Mwanza kuhusu matumizi sahihi na salama ya nishati ya umeme, lengo likiwa ni kuhakikisha ajali zitokanazo na matumizi ya umeme yasiyo sahihi zinatokomezwa.

Warsha hiyo imefanyika Februari Mosi 2020 katika Ofisi za TANESCO Igogo jijini Mwanza ambapo Viongozi hao wamehimizwa kufikisha kwa wananchi elimu waliyoipata ikiwemo kuepuka uharibifu wa miundombinu ya umeme kama vile kuchoma nguzo, kujenga kwenye mkondo wa umeme, kufanya shughuli za biashara jirani na nyaya ama transfoma za umeme.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Mhandisi Godfrey Vomo akifungua warsha kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa jijini mwanza iliyolenga kuwaelimisha matumizi sahihi na salama ya nishati ya umeme ili nao wakawaelimishe wananchi katika Mitaa yao.
 Afisa wa Usalama Mahala pa Kazi TANESCO Mkoa Mwanza, Mhandisi Julius Venance akiwasilisha mada ya usalama na matumizi sahihi ya nishati ya umeme kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa jijini Mwanza.
 Afisa Uhusiano (Elimu kwa Umma) TANESCO Mkoa Mwanza, Flaviana Moshi akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusiana na matumizi sahihi ya nishati ya umeme kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa jijini Mwanza.
Afisa Uhusiano Msaidizi (Elimu kwa Umma) TANESCO Mkoa Mwanza, Lilian Mungai akitoa ufafanuzi kuhusu kifaa cha UMETA kinachorahisisha mteja kuunganishiwa huduma ya umeme bila kufanya 'wiring'.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa NHC Magharibi jijini Mwanza, Jumanne Maganga amesema elimu kuhusu matumizi sahihi ya nishati ya umeme pamoja na usalama itawasaidia katika utendaji kazi wao huku akipendekeza TANESCO kuandaa mabango yanayotoa elimu hiyo ili kuyaweka katika maeneo ya wazi wananchi wajisomee pia.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyasaka Manispaa ya Ilemela, Grace Bilikwija akitoa pongezi kwa TANESCO kutokana na umuhimu wa elimu waliyoipata na kuahidi kuifikisha kwa wananchi.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.