LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella azindua zoezi la upuliziaji dawa ya ukoko wilayani Ukerewe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amezindua rasmi zoezi la upuliziaji dawa ya ukoko katika makazi na mazalia ya mbu wilayani Ukerewe ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa afua mbalimbali za kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.

Akizungumza Machi 09, 2020 na wakazi wa Kata ya Ngoma baada ya kuzindua zoezi hilo, Mongella aliwahimiza wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwani dawa hiyo haina madhara yoyote kwa binadamu.

Serikali inashirikiana na taasisi ya “ABT Associates” kutekeleza mradi wa unyunyiziaji dawa ya kuua mazalia ya mbu (PMI VectorLink) kupitia ufadhili wa wadau mbalimbali ikiwemo US Aid, CDC pamoja na mfuko wa kupambana na Malaria wa Rais wa Marekani.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akinyunyizia dawa ya ukoko kwa ajili ya kuua mazalia ya mbu katika nyumba ya mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Hamkoko wilayani Ukerewe.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.