LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watetezi watoa tamko “tukio la binti aliyeuawa na mwajiri wake Arusha”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Watetezi wa Haki za Binadamu hususani wafanyakazi wa nyumbani wametoa tamko la kulaani tukio la mfanyakazi wa nyumbani jijini Arusha Salome Zakaria (19) anayedaiwa kupigwa na mwajiri wake Mkami Shirima na kumsababishia kifo.

Tamko la watetezi hao limesomwa Machi 13, 2020 na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani (WoteSawa), Angela Benedicto akiwakilisha mashirika mengine ambayo ni Tanzania Domestic Coalition (TDWC), Kiota Women Health and Development Organization (KIWOHEDE), Mwanza Youth and Children Network (MYCN), Ndenuka Organization, Haki Zetu Organization, Nuru Organization, HAWA & Wanawake Live pamoja na Binti Inuka Organization.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.