Wasiojiweza wasaidiwa gharama za matibabu katika Hospitali ya Bugando
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Baadhi ya wanafunzi
waliowahi kusoma katika Shule ya Sekondari Makoko Seminari (Makoko Seminary)
iliyopo Musoma mkoani Mara, wametoa msaada wa fedha ili kusaidia gharama za matibabu
kwa wagonjwa wenye uhitaji katika Hospitali ya Kanda Bugando jijini Mwanza.
Waseminari
hayo walikabidhi msaada huo kwa niaba ya wenzao Jumatatu Aprili 13, 2020 huku
ikielezwa kuwa gharama za wagonjwa wasiojimudu kiuchumi ambao wanaoomba msamaha wa matibabu katika
hospitali ya Bugando zinafikia milioni 200 kila baada ya miezi mitatu hivyo ni vyema wadau mbalimbali wakaendelea kusaidia upatikanaji wa gharama hizo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Badhi ya wanafunzi waliowahi kusoma Shule ya Sekondari Makoko Seminari (Makoko Seminary) iliyopo Musoma mkoani Mara wakifanya maombi baada ya kuwasili katika Hospitali ya Kanda Bugando kuwasilisha msaada wa fedha kwa ajili ya kugharamia matibabu kwa wagonjwa wenye uhitaji.
Badhi ya wanafunzi waliowahi kusoma Shule ya Sekondari Makoko Seminari (Makoko Seminary) iliyopo Musoma mkoani Mara wakiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Hospitali ya Kanda Bugando baada ya kukabidhi msaada wa fedha katika Hospitali hiyo kwa ajili ya kusaidia gharama za matibabu kwa wagonjwa wasiojimudu kiuchumi.
Badhi ya wanafunzi waliowahi kusoma Shule ya Sekondari Makoko Seminari (Makoko Seminary) iliyopo Musoma mkoani Mara wakiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Hospitali ya Kanda Bugando.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: