LIVE STREAM ADS

Header Ads

Uboreshaji daftari la wapiga kura “NEC yaonya unyanyapaa”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Maafisa wasimamizi wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura wametakiwa kuzingatia tahadhari za kiafya dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona huku wakitimiza majukumu yao bila kuwanyanyapaa wananchi.

Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alitoa rai hiyo Jumatano Aprili 15, 2020 wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura awamu ya pili katika Jimbo la Nyamagana.

Mafunzo hayo yalihusisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata, Waandishi Wasaidizi pamoja na Wasimamizi wa Mashine (BVR KIT Operator) ambao pia walikula kiapo cha kujitoa uanachama ama kutokuwa na chama chochote cha siasa kilichoongozwa na Hakimu Mkazi Mkoa Mwanza, Boniventure Lema.

Awamu ya pili ya uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura limepangwa kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza kuanzia Aprili 17-19, 2020.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akisisitiza jambo kwenye mafunzo hayo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 Maafisa na Watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakila kiapo cha kujitoa uanachama ama kutokuwa na chama chochote cha siasa ili kusimamia vyema zoezi la uboreshaji daftari la wapiga kura.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.